Paula Frassinetti
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Paula Frassinetti (Genova, 3 Machi 1809 - Roma, 11 Juni 1882[1]) alikuwa bikira wa Italia kaskazini ambaye, kwa kushinda matatizo mengi, alianzisha shirika la Masista wa Mt. Dorothea kwa ajili ya malezi ya wasichana na mayatima[2], akaliongoza kwa ushujaa na upole[3].

Kwa sasa masista wake wako 1,200 katika Ulaya, Afrika, Asia na Amerika ya Kilatini[4].
Papa Pius XI alimtangaza mwenye heri tarehe 8 Juni 1930 na Papa Yohane Paulo II mtakatifu tarehe 11 Machi 1984.
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads