Paulo Hanh
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Paulo Hanh (kwa Kivietnam: Phaolô Hạnh; Chợ Quán, Vietnam, 1826 hivi - Saigon, Vietnam, 28 Mei 1859) alikuwa Mkristo ambaye, baada ya kupuuzia maadili, aliongoza kikundi cha majambazi.
Alipokamatwa chini ya kaisari Tu Duc, alikiri kwa ushujaa imani yake bila kujali mabembelezo, vitisho na mateso hata akakatwa kichwa[1] na hivi kuwa mmojawapo kati ya Wakristo wafiadini wa Vietnam waliouawa kwa ajili ya imani yao huko Vietnam katika karne ya 17, 18 na 19 (1625–1886).
Wanatajwa pia kama Watakatifu Andrea Dũng-Lạc na wenzake 116.
Kwa nyakati tofauti, Papa Leo XIII, Papa Pius X na Papa Pius XII waliwatangaza kuwa wenye heri, halafu Papa Yohane Paulo II aliwaunganisha katika kuwafanya watakatifu wafiadini tarehe 19 Juni 1988.
Sikukuu yao huadhimishwa kwa pamoja kila tarehe 24 Novemba. Paulo Hahn anaadhimishwa pia tarehe 28 Mei, ambapo ndipo alipouawa akiwa mlei[2].
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Marejeo ya Kiswahili
Marejeo ya lugha nyingine
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads