Perth

From Wikipedia, the free encyclopedia

Perthmap
Remove ads

Perth ni mji mkuu wa jimbo la Australia Magharibi uliopo kwenye kingo za Mto Swan.

Ukweli wa haraka
Thumb
Mahali pa Perth nchini Australia

Kuna wakazi karibu watu milioni 2.1 wanaoishi katika jiji hilo. [2] Ni mji mkubwa wa nne huko Australia, baada ya Sydney, Melbourne na Brisbane.

Perth ilianzishwa mnamo 1829 na nahodha James Stirling; huyu baharia alikuwa mwenyeji wa Uskoti hivyo alitumia jina la mji Perth wa Uskoti.

Perth ni maarufu kwa mchanga wake mweupe, mweupe. Fukwe zake ni bora kwa kuogelea. Kivutio maarufu cha watalii cha ndani ni Kisiwa cha Rottnest, ambacho kinakaliwa na wanyama wadogo wa kienyeji wanaoitwa Quokkas. Kivutio kingine maarufu ni Kings Park, ambayo ni mojawapo ya mbuga kubwa za jiji ulimwenguni.

Remove ads

Vyuo vikuu

Perth ina vyuo vikuu vifutavyo: [3]

  • Chuo Kikuu cha Australia Magharibi
  • Chuo Kikuu cha Murdoch
  • Chuo Kikuu cha Curtin
  • Chuo Kikuu cha Edith Cowan
  • Chuo Kikuu cha Notre Dame (Australia Magharibi) (kibinafsi)

Tabianchi

Tabianchi ni nusutropiki, kuna kipindi cha joto ambako hasa Januari na Februari hufikia viwango vya zaidi ya °C 31. Kinyume chake kuna miezi inayofanana na eneo la Mediteranea, katika miezi ya Juni hadi Agosti jotoridi hushuka chini °C 20 na kiasi cha mvua kinazidi milimita 120; jalidi (chini ya °C 0) hutokea mara chache. [4] [5] [6]

Marejeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads