Peter Chanel
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Petro Shanel (Cuet, Ufaransa, 12 Julai 1803 – Futuna, Oseania, 28 Aprili 1841) alikuwa padri mmisionari wa Kanisa Katoliki.

Ametambuliwa rasmi na Papa Leo XIII kuwa mwenye heri tarehe 17 Novemba 1889, halafu na Papa Pius XII kuwa mtakatifu kama mfiadini tarehe 12 Juni 1954.
Maisha
Baada ya kupata upadrisho alishughulika na uchungaji nchini mwake kwa miaka michache, akiwajibika hasa kwa ajili ya wakulima na malezi ya vijana.
Halafu aliingia Shirika la Maria, akatumwa akatumwa katika visiwa vya Oceania pamoja na wenzake kadhaa kuhubiri Injili mahali ambapo ilikuwa haijatangazwa.
Licha ya matatizo mengi alifaulu kwa upole wake kuwaongoa watu kadhaa katika kisiwa cha Futuna, akiwemo mwana wa mfalme. Kwa sababu ya kuchukiwa kwa imani ya Ukristo, huyo kwa hasira aliagiza akamatwe na kuuawa kwa kupigwa rungu [2].
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads