Australia na Pasifiki

eneo la kijiografia linalojumuisha Australasia, Melanesia, Micronesia na Polynesia From Wikipedia, the free encyclopedia

Australia na Pasifiki
Remove ads

Australia na Visiwa vya Pasifiki (pia: Oceania, Okeania, Oshania) hujumlishwa mara nyingi pamoja katika hesabu ya mabara.

Thumb
Ramani ya Australia na Visiwa vya Pasifiki
* AS: Samoa ya Marekani * AU: Australia * CK: Visiwa vya Cook * FJ: Fiji * FM: Mikronesia * GU: Guam (USA) * KI: Kiribati * MH: Visiwa vya Marshall * MP: Visiwa vya Mariana * NC: Kaledonia Mpya (Ufaransa) * NR: Nauru * NU: Niue (New Zealand) * NZ: New Zealand * PF: Polynesia ya Kifaransa * PG: Papua Guinea Mpya * PN: Pitcairn (Uingereza) * PW: Palau * SB: Visiwa vya Solomon * TL: Timor ya Mashariki * TK: Tokelau * TO: Tonga * TV: Tuvalu * US: Hawaii * VU: Vanuatu * WF: Wallis na Futuna (Ufaransa) * WS: Samoa ya Magharibi Nchi za Asia * [BN]: Brunei * [CN]: China * [ID]: Indonesia * [MY]: Malaysia * [PH]: Ufilipino * [TW]: Taiwan

Hasa watu kwenye visiwa vingi vya Pasifiki wana utamaduni wa karibu. Vilevile historia ya visiwa hivyo kabla ya kuenea kwa ukoloni imefanana katika mengi.

Remove ads

Bara au la?

Hivyo mara nyingi sehemu hii ya dunia imeitwa "Bara la Kiutamaduni". Jina hili si sahihi kijiografia kwa sababu maeneo yake yako juu ya mabamba ya gandunia tofauti, kama vile bamba la Pasifiki, bamba la Australia na mengine madogo. Hata wataalamu hawapatani kuhusu mipaka ya eneo hilo.

Jina

Kwa lugha nyingi za dunia jina la "Oceania" (Okeania, Oshania) limekuwa la kawaida kutokana na neno la Kigiriki "okeanos" (kwa Kilatini: oceanus; kwa Kiingereza: ocean). Hivyo "Oceania" yamaanisha "nchi katika bahari". Ila tu hatuoni faida ya kuingiza neno hili katika lugha ya Kiswahili kwa sababu ni neno lisiloeleweka vizuri. Mara wataalamu hujadili "Oceania" kuwa visiwa vya Pasifiki pamoja na Australia; mara wanaona "Oceania" ni visiwa vile pekee bila Australia na wengine wanasema wenyewe "visiwa vya Pasifiki" ingekuwa jina zuri zaidi kama Australia haihesabiwi.

"Australasia" imekuwa jaribio tofauti la kutaja eneo, hasa kati ya wataalamu wa Australia, ila tu halipendwi na watu wengi visiwani. Hivyo imetumiwa zaidi kwa kanda la Australia na visiwa jirani pekee.

Remove ads

Eneo

Visiwa vyote kwa pamoja (bila Australia yenyewe) hukadiriwa kuwa 7,500 vyenye eneo la nchi kavu la kilomita za mraba milioni 1.3 vilivyosambaa katika eneo la bahari la kilomita za mraba milioni 70. Takriban visiwa 2,100 vimekaliwa na watu milioni 14.9.

Jiolojia

Eneo hili si bara kwa maana ya jiolojia. Visiwa vikubwa vya New Zealand, Guinea Mpya, Kaledonia Mpya na Tasmania ni mabaki ya bamba la Gondwana ya kihistoria. Guinea Mpya imetenganishwa na Australia kwa bahari ya Arafura isiyo na kina kirefu na wakati wa enzi ya barafu iliyopita zilikuwa kama nchi moja kwa sababu uwiano wa bahari ulikuwa chini kuliko leo.

Visiwa vingi katika Pasifiki ni milima ya volkeno inayoinuka kutoka tako la bahari hadi uso wa maji; mara nyingi zinaonyesha kasoko. Visiwa vingine vinajengwa na matumbawe yanayokua juu ya volkeno ambazo zimeishia kidogo chini ya uso wa bahari. Visiwa vingine ni atoli ambako matumbawe yamejenga tuta tumbawe kwa umbo la mviringo kuzunguka kisiwa cha kivolkeno.

Sababu ya kutokea kwa volkeno nyingi ni miendo ya gandunia katika tabaka za ganda la dunia chini ya bahari. Ngozi ya nje au ganda la dunia hufanywa na vipande mbamlimbali (=mabamba ya gandunia) vinavyoelea juu ya tabaka ya mwamba moto na kiowevu. Pale ambako vipande hivi vinagusana mara kwa joto na mwamba moto ulioyeyuka unapanda juu; pale ambao kupanda huku kunatokea haraka tunaona volkeno na hivyo kisiwa kipya kutokea. Mfano ni safu ya visiwa vya Hawaii ambavyo ni safu ya milima ya volkeno inayoanza kwenye tako la bahari, mengine inaonekana kama visiwa, mengine iko chini ya uso wa bahari.

Remove ads

Historia

Angalia Historia ya maeneo ya Pasifiki na Historia ya Australia

Kanda

Mara nyingi kanda nne zimetofautishwa:

Maeneo yanayotajwa kwa "Melanesia" na "Australasia" huingiliana.

Nchi na Maeneo ya Australia na Visiwa vya Pasifiki

(Nchi huru zaonekana kwa mwandiko mzito, maeneo yaliyo chini ya nchi nyingine kwa mwandiko wa kawaida)

Maelezo zaidi Jina la eneo, pamoja na bendera, Eneo (km²) ...
Remove ads

Tanbihi

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads