Petro Dong
baba wa familia ambaye alikubali kuteswa kwa ukatili kuliko kukanyaga msalaba From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Petro Dong (1800 - 1862) alikuwa baba wa familia ambaye alikubali kuteswa kwa ukatili kuliko kukanyaga msalaba. Alipoagizwa achanjwe usoni neno “dini ya uongo” aliandikishwa “dini ya ukweli” akakatwa kichwa kwa hilo chini ya kaisari Tu Duc[1].
Ni mmojawapo kati ya Wakristo wafiadini wa Vietnam waliouawa kwa ajili ya imani yao huko Vietnam katika karne ya 17, 18 na 19 (1625–1886).
Wanatajwa pia kama Watakatifu Andrea Dũng-Lạc na wenzake 116.
Kwa nyakati tofauti, Papa Leo XIII, Papa Pius X na Papa Pius XII waliwatangaza kuwa wenye heri, halafu Papa Yohane Paulo II aliwaunganisha katika kuwafanya watakatifu wafiadini tarehe 19 Juni 1988.
Sikukuu yao huadhimishwa kwa pamoja kila tarehe 24 Novemba, lakini ya kwake mwenyewe tarehe 3 Juni[2].
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Marejeo
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads