Pilot (sehemu ya Prison Break)

From Wikipedia, the free encyclopedia

Pilot (sehemu ya Prison Break)
Remove ads

"Pilot" ni sehemu ya kwanza kabisa ya mfululizo wa tamthilia ya kusisimua ya Kimarekani Prison Break. Sehemu hii imeongozwa na Brett Ratner na kutungwa na Paul Scheuring, ambaye pia ni muundaji wa mfululizo huu. Ilionyeshwa kwa mara ya kwanza nchini Marekani mnamo Agosti 29, 2005, kwenye kituo cha televisheni cha Fox. Sehemu hii inamtambulisha Michael Scofield (uhusika uliochezwa na na Wentworth Miller), ambaye anajiingiza kwa makusudi jela la Fox River State ili kumnasua kaka yake, Lincoln Burrows (uhusika ulichezwa na Dominic Purcell), ambaye alihukumiwa kifo kwa kosa la mauaji ya kaka wa Makamu wa Rais. Kosa ambalo hakulitenda.

Ukweli wa haraka "", Sehemu ya Prison Break ...
Remove ads

Muhtasari

Baada ya kujichora machata korofi yanayoleta ramani ya gereza na maelezo mengine ya siri, Michael Scofield anajiingiza mwenyewe jela kwa kupora benki. Mara tu anapofika gerezani, anakutana na Lincoln Burrows na kuanza kutekeleza mpango wake wa kumtorosha Lincoln kabla ya tarehe yake ya kunyongwa. Michael anaanza kutathmini mazingira ya gereza, kukusanya washirika, na kutafuta njia ya kufikia maeneo muhimu kwa ajili ya kutoroka. Anapambana na changamoto za utawala wa gereza, walinzi, na magenge mbalimbali ya wafungwa, huku akijaribu kuficha nia yake halisi kutoka kwa kila mtu.

Remove ads

Hadithi

Sehemu ya "Pilot" inaanza kwa kuanzisha njama kuu ya Prison Break: mhandisi Michael Scofield akijaribu kumuokoa kaka yake kutoka kipengele cha kunyongwa. Michael anaonekana akiwa na chata lake kubwa mgongoni na mikononi, iliyoundwa kuficha ramani na namba muhimu zitakazomsaidia kutoroka. Tunaona jinsi anavyopora benki kwa makusudi ili ahukumiwe na kupelekwa Fox River.

Gerezani, Michael anakutana na Lincoln Burrows na wanafanya "mazungumzo" yao ya kwanza kama wafungwa. Michael anaanza kuchunguza njia za kutoroka, akijifanya anatumia ujuzi wake wa uhandisi kurekebisha mambo gerezani. Anawasiliana na wafungwa wengine muhimu kama vile Fernando Sucre (mjelamjela mwenza), John Abruzzi (mkuu wa Mafia anayeweza kutoa ndege), na Theodore "T-Bag" Bagwell (mfungwa hatari anayeweza kuleta matatizo). Pia, anakutana na Daktari Sara Tancredi, ambaye anafanya kazi katika kliniki ya gereza, eneo muhimu kwa mpango wake. Mwishoni mwa kipindi, Michael anaanza kutekeleza hatua ya kwanza ya mpango wake, akionyesha utatuzi wa matatizo yake na akili yake ya hali ya juu.

Remove ads

Marejeo

Viungo vya Nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads