Piniani

From Wikipedia, the free encyclopedia

Remove ads

Piniani (Roma, Italia, 381 hivi - Yerusalemu, Israeli/Palestina, 31 Desemba 420 hivi) alikuwa Mkristo wa mmojawapo kati ya koo maarufu zaidi za mji huo.

Alimuoa mapema Melania Kijana,mwanamke Mkristo wa mwingine kati ya koo maarufu zaidi za mji huo, akazaa watoto wawili na walipofiwa nao, walikubaliana kuishi kama watawa.

baada ya kurithi mali ya wazazi waliofariki, waliitoa kwa Kanisa na kwa maskini[1] wakaelekea Sisilia (408), halafu Afrika (410) walipofunga urafiki na Augustino wa Hippo na kuanzisha monasteri dabo[2].

Mwaka 417 walihamia Nchi Takatifu kwenye Mlima wa Mizeituni walipoanzisha tena monasteri na kuishi huko hadi kifo [3].

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu pamoja na mkewe.

Sikukuu yao ni tarehe 31 Desemba[4].

Remove ads

Tazama pia

Tanbihi

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads