Quodvultdeus
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Quodvultdeus (jina la Kilatini lenye maana ya "Anachotaka Mungu"; alifariki Napoli, Italia, mwaka 450 hivi) alikuwa Mberberi aliyehudumia kama askofu wa Karthago (katika Tunisia ya leo) tangu mwaka 435 hadi 439 alipofukuzwa na mfalme Genseriki wa Wavandali Waario alipoteka mji huo. Yeye na waklero wake walipandishwa juu ya meli chakavu zisizo na tanga wala makasia, kumbe walifika salama nchini Italia alipohamia hadi kifo chake[2][3].

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 19 Februari[4]; lakini pia 8 Januari, 26 Oktoba au 28 Novemba[5].
Remove ads
Maisha
Mwaka 407 alikuwa akiishi Karthago akawa shemasi mwaka 421. Aliongozwa kiroho na Augustino wa Hippo[3] ambaye alimtolea baadhi ya maandishi yake.[3]
Maandishi

Baadhi ya maandishi yake mwenyewe yametufikia, zikiwemo hotuba 12, kati yake 3 juu ya Kanuni ya Imani (kilichotafsiriwa katika Kiingereza kama The Creedal Homilies: conversion in fifth-century North Africa, Thomas Macy Finn (translation and commentary), New York : Newman Press, 2004, p. 137.
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads