Riksho
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Riksho (pia: riksha; kwa Kiingereza: rickshaw; kutoka neno la Kijapani) ni chombo cha usafiri ambacho kiasili kilikuwa gari dogo lenye kiti lililovutwa na mtu, ilhali abiria amekalia nyuma.



Historia
Riksho ya kwanza ilitengenezwa mwaka wa 1869 nchini Japani. Taarifa zinatofautiana kama mvumbuzi alikuwa mwenyeji wa Japani au mgeni kutoka Ulaya[1] au Marekani [2].
Zilienea haraka katika nchi za Asia. Riksha za kuvutwa zilipokelewa vizuri mno na watu wa Asia katika karne ya 19 huku vijana wengi wakijitosa katika ajira za kuvuta riksha hizi. Mnamo mwaka 1920 kulikuwa na riksha 60,000 mjini Beijing (China) na takriban mmoja kati ya wanaume sita katika mji huu alifanya kazi ya kuvuta chombo hiki[3].
Baadaye riksho ziliendelea kuunganishwa na baisikeli ilhali dereva moja anaendesha baisikeli ya magurudumu matatu ambako abiria hukalia ama mbele ama nyuma ya dereva. Tangu kuenea kwa pikipiki mfumo huu ulibadilishwa kuwa pia na injini ya petroli. Riksho za pikipiki ziliendelea kupata chumba kidogo cha abiria na hivyo zinajulikana kwa jina la tuk-tuk katika sehemu kadhaa za Asia, pia kwa jina la bajaj nchini Uhindi na kutoka huko zilifika kama "bajaji" katika Afrika ya Mashariki.
Riksho asilia za kuvutwa zinapatikana bado katika miji michache lakini idadi inapungua haraka.
Remove ads
Tanbihi
Marejeo
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads