Beijing

From Wikipedia, the free encyclopedia

Beijing
Remove ads

Beijing (pia: Peking) ni mji mkuu wa China. Uko kaskazini-mashariki mwa nchi. Kiutawala jiji la Beijing pamoja na maeneo ya jirani hutawaliwa kama mkoa wa nchi wenye eneo la km² 16,800. Tangu karne sita imekuwa kitovu cha utawala wa China. Jina lenyewe lamaanisha "Mji Mkuu wa Kaskazini" kwa sababu China iliwahi kuwa na vitovu mbalimbali hasa Nanjing (mji mkuu wa kusini). Kutokana na historia ndefu kuna majengo mengi mazuri yanayohifadhiwa hata kama mitaa mingine inabadilika haraka. Sehemu inayohifadhiwa ni pamoja na Uwanja wa Tianamen, Mji Haramu pamoja na nyumba za makaisari wa China na mahekalu mbalimbali.

Ukweli wa haraka Nchi ...
Thumb
Beijing

Rundiko la jiji lina wakazi wapitao milioni 22. Hivyo leo hii Beijing ni mji mkubwa wa tatu katika China baada ya Chongqing na Shanghai. Katika historia iliwahi kuwa mji mkubwa zaidi duniani katika karne ya 13 hadi ya 18.

Mwaka 2008 Beijing ilikuwa mwenyeji wa michezo ya Olimpiki.

Remove ads

Picha


Viungo vya nje

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu maeneo ya China bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Beijing kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads