Robati Southwell
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Robati Southwell, S.J. (Norfolk, Uingereza, 1561 hivi – Tyburn, London, 21 Februari 1595) alikuwa padri wa Kanisa Katoliki ambaye kwa sababu hiyo aliuawa na serikali ya nchi yake.
Alikuwa pia mshairi wa lugha ya Kiingereza akatunga tenzi za kidini.
Papa Pius XI alimtangaza mwenye heri tarehe 15 Desemba 1929 halafu Papa Paulo VI tarehe 25 Oktoba 1970 alimtangaza kuwa mtakatifu mfiadini pamoja na wenzake 39[1].
Remove ads
Maisha
Robati alikwenda kusoma Ufaransa akajiunga na Wajesuiti huko Roma, Italia, mwaka 1578. Hukohuko aliendelea na masomo ya falsafa na teolojia akapata upadirisho (1584).
Baada ya kufundisha huko miaka miwili aliomba kurudi kwao ingawa serikali ilikuwa inadhulumu Wakatoliki. Alifanya uchungaji hasa London kwa miaka sita hadi alipokamatwa na hatimaye kuuawa kwa kuchanwachanwa kikatili kuteswa kikatili kwa amri ya malkia Elizabeti I mwenyewe na kuuawa kwa kunyongwa chini ya sheria [3].
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Marejeo
Marejeo mengine
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads