Wilaya ya Rufiji

From Wikipedia, the free encyclopedia

Wilaya ya Rufiji
Remove ads

Wilaya ya Rufiji ni wilaya mojawapo ya Mkoa wa Pwani yenye postikodi namba 61600.

Thumb
Mkoa wa Pwani na Wilaya ya Rufiji.

Katika sensa ya mwaka 2002, idadi ya wakazi wa wilaya hiyo ilihesabiwa kuwa 92,602 [1], walioongezeka kuwa 217,274 wakati wa sensa ya mwaka 2012[2]. Katika sensa ya mwaka 2022 walihesabiwa 159,906 [3].

Wilaya ya Rufiji imegawanyika sehemu mbili, visiwani na bara: wenyeji wa visiwani ni wa kabila la Wanyagatwa na walio bara ni Wamatumbi, Warufiji na Wandengereko. Wenyeji wa visiwani wanajishughulisha sana na uvuvi, kilimo cha mnazi na kupika chumvi, wakati wale wengine wanajishughulisha sana na mazao ya vyakula kama vile mpunga, mahindi n.k.

Makao makuu ya wilaya yanapatikana Utete.

Remove ads

Marejeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads