Salome (mke wa Zebedayo)

From Wikipedia, the free encyclopedia

Salome (mke wa Zebedayo)
Remove ads

Salome (kwa Kiebrania: שלומית, Shelomit, kutoka mzizi שָׁלוֹם, shalom, yaani amani[1]) alikuwa mke wa Zebedayo na mfuasi wa Yesu Kristo pamoja na wanae Yakobo Mkubwa na Mtume Yohane, waliokuwa marafiki wakuu wa Yesu pamoja na mtume Petro.

Thumb
Picha takatifu ya Kiorthodoksi ya Salome na wenzake kwenye Kaburi la Yesu (Kizhi, karne ya 18).

Kwa msingi huo alithubutu kumuomba Yesu awape wanae nafasi mbili za kwanza katika ufalme wake ujao.

Anatajwa kati ya wanawake waliosimama chini ya Yesu msalabani (Mk 15:40; Math 27:56) na kati ya wale waliowahi kwenda kaburini Jumapili asubuhi na mapema (Mk 16:1)[2].

Pengine anadhaniwa kuwa na undugu na Bikira Maria, mama wa Yesu.[3]

Anaheshimiwa na madhehebu mengi ya Ukristo kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 24 Aprili.[4]

Remove ads

Picha

Tazama pia

Tanbihi

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads