Seaborgi

From Wikipedia, the free encyclopedia

Seaborgi
Remove ads

Seaborgi (kwa Kiingereza: seaborgium) ni elementi sintetiki iliyo na alama Sg na namba atomia 106. Imepokea jina lake kwa heshima ya mwanakemia wa Marekani Glenn T. Seaborg . Ilhali ni elementi sintetiki, haitokei kiasili katika mazingira yetu lakini inaweza kuundwa katika maabara. Ni dutu nururifu; isotopi yake iliyo thabiti zaidi inaitwa 269 Sg, ikiwa na nusumaisha ya dakika 14 hivi.


Ukweli wa haraka Seaborgi (seaborgium) ...

Atomu za kwanza za seaborgi zilitengenezwa mwaka 1974 katika maabara huko Umoja wa Kisoyeti na Marekani. Pande hizo mbili zilivutana kwa miaka kadhaa kuhusu nani aliwahi kuigundua na haki ya kuamulia jina, hadi mwaka 1997 Jumuiya ya Kimataifa ya Kemia (IUPAC) iliamua jina rasmi kuwa "seaborgium".

Tabia nyingi za elementi hiyo hazijulikani kwa sababu mbili

a) elementi hii inapatikana tu baada ya kutengenezwa katika maabara kwa gharama kubwa [1]

b) baada ya kupatikana inaachana haraka, haidumu

Thumb
Elementi 106 ilipewa jina la Glenn T. Seaborg, mtafiti wa elementi sintetiki, kwa jina seaborgium (Sg).

[2]

Remove ads

Marejeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads