Sesari wa Nazianzo

From Wikipedia, the free encyclopedia

Sesari wa Nazianzo
Remove ads

Sesari wa Nazianzo (Arianzo, leo Güzelyurt, mkoani Kapadokia, katikati ya nchi ambayo leo inaitwa Uturuki, 331 hivi - Nazianzo, 369 hivi) alikuwa mganga wa ikulu[1][2][3].

Thumb
Picha takatifu ya Mt. Sesari.

Tangu zamani anaheshimiwa na Kanisa Katoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu[4].

Sikukuu yake inaadhimishwa tarehe 25 Februari[5].

Maisha

Alizaliwa katika familia ya kisharifu ya watakatifu. Baba yake aliitwa Gregori mzee na mama yake Nonna. Kaka yake alikuwa Gregori wa Nazienzi.

Baba, aliyekuwa Myahudi, aliongokea Ukristo kwa msaada wa mke wake na hatimaye akawa askofu wa Nazianzo.

Hata hivyo Sesari alibatizwa tu muda mfupi kabla hajafa kwa tauni, baada ya kunusurika kufa katika tetemeko la ardhi lililopata mji wa Nisea alipokuwa afisa wa serikali.

Alikuwa amesoma fani mbalimbali kwanza huko Kaisarea wa Kapadokia, halafu Aleksandria ya Misri, alipowazidi wanafunzi wenzake wote[6].

Remove ads

Tazama pia

Tanbihi

Vyanzo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads