Simeoni wa Mnarani

From Wikipedia, the free encyclopedia

Simeoni wa Mnarani
Remove ads

Simeoni wa Mnarani (kwa Kisiria: ܫܡܥܘܢ ܕܐܣܛܘܢܐ, šamʻun dasṯonáyá, kwa Kigiriki: Συμεών ὁ στυλίτης, Symeón o Stylítis; kwa Kiarabu سمعان العمودي, Simʿān al-ʿAmūdī; kwa Kiingereza: Symeon the Stylite; Sis (leo nchini Uturuki), 390 hivi - Qalaat Semaan, Syria, 2 Septemba 459[1][2]) alikuwa mkaapweke kutoka Assyria aliyepata umaarufu kwa kuishi kiadilifu sana miaka 37 juu ya mnara karibu na Aleppo[3][4][5][6].

Thumb
Picha takatifu ya Mt. Simeoni huko Sanok, Polandi.

Pengine anaongezewa sifa "mzee" ili kumtofautisha na waliofuata mtindo wake huo kama Simeoni wa Mnarani Kijana, Simeoni wa Mnarani III na Simeoni wa Mnarani wa Lesbos.

Tangu kale anaheshimiwa na Waorthodoksi, Waorthodoksi wa Mashariki, Wakatoliki na Waanglikana kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 27 Julai[7], 5 Januari, 1 Septemba au nyingine kadiri ya madhehebu.

Remove ads

Tazama pia

Tanbihi

Marejeo ya Kiswahili

Marejeo ya lugha nyingine

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads