T-Pain

From Wikipedia, the free encyclopedia

T-Pain
Remove ads

Faheem Rasheed Najm (anafahamika zaidi kwa jina la kisanii kama T-Pain; amezaliwa 30 Septemba 1985) ni mwimbaji, mtunzi, rapa, na mtayarishaji wa rekodi kutoka Marekani.

Ukweli wa haraka Maelezo ya awali, Jina la kuzaliwa ...
Remove ads

Wasifu

Najm alizaliwa mjini Tallahassee, Florida.[1] Jina lake la kisanii ni kifupi cha "Tallahassee Pain" ("Tallahassee Mauimivu) na amechagua jina hilo kwa sababu ya ugumu wa maisha aliyoyapata wakati anaishi huko.[2]

Alianza shughuli za urapa akiwa katika kundi la Nappy Headz. Mnamo mwaka wa 2005, akawa mwimbaji na kuweza kutoa albamu yake ya kwanza iliyoitwa Rappa Ternt Sanga ikiwa na vibao vyake vikali vya "I'm Sprung" na "I'm N Luv (Wit A Stripper)".

Shughuli zake kama mwimbaji, T-Pain ametumia sana kionjo cha sauti cha Auto-Tune. Tangu kutolewa kwa albamu yake ya kwanza, T-Pain ametayarisha vibao kadhaa vikali vyake mwenyewe na vya marapa na waimbaji wengine wa R&B. T-Pain pia amekuwa na single kumi kwenye chati za Billboard Hot 100. Mnamo mwaka wa 2008, ameshinda tuzo ya Grammy na rapa Kanye West kwa ajili ya single ya "Good Life". Mnamo mwaka wa 2010 ameshinda tuzo nyingine ya Grammy na Jamie Foxx kwa ajili ya single ya "Blame It". T-Pain pia ni mwanzilishi wa studio ya kurekodia ya Nappy Boy Entertainment, imeanzishwa mwaka wa 2005.

Remove ads

Kazi

Diskografia

Makala kuu: Diskografia ya T-Pain
Single zake

Marejeo

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads