Thomas Becket
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Thomas Becket (Cheapside, London, Uingereza, 1118 (au 1120) – 29 Desemba 1170) alikuwa Askofu mkuu wa Canterbury tangu 1162 hadi kifodini chake kilichotokea wakati wa Misa katika kanisa kuu.

Sababu ya kuuawa ni kubishana kwake na mfalme Henri II wa Uingereza juu ya haki na juu ya fadhili za Kanisa.
Kwa ajili hiyo alikuwa ameshafukuzwa kutoka jimbo lake na kutoka ufalme wote wa Uingereza.
Baada ya miaka sita aliweza kurudi nchini, lakini aliendelea kusumbuliwa sana hadi alipomuendea Kristo kwa kuchomwa na askari wa mfalme kwa upanga [1].
Muda mfupi baadaye Papa Alexander III alimtangaza mtakatifu mfiadini tarehe 21 Februari 1173. Ndivyo anavyoheshimiwa na Kanisa Katoliki na Anglikana.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 29 Desemba[2].
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Marejeo ya Kiswahili
Marejeo ya lugha nyingine
Marejeo mengine
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads