Thug Life: Volume 1
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Thug Life: Volume 1 ilikuwa albamu ya kwanza kutolewa na kundi la Thug Life, lililoanzishwa na rapa Tupac Shakur, na ilitolewa mnamo tar. 26 Septemba 1994. Awali albamu ilitolewa na studio ya Shakur ya Out Da Gutta Records. Kwa kufuatia upondaji mkubwa juu ya muziki wa gangsta rap kwa kipindi hicho, toleo halisi la albamu likatiwa kapuni na kurekodiwa upya na nyimbo nyingine mpya kibao na zile baadhi za awali kukatwa. Ilisemekana kwamba 2Pac alitengeneza matoleo mengine mawili ya albamu hii, yenye nyimbo kibao ambazo bado hazikutolewa. Kundi linaunganishwa na Big Syke, Macadoshis, Mopreme, The Rated R na Tupac Shakur. Miongoni mwa nyimbo kali kutoka kwenye albamu hii ni pamoja na "Bury Me a G","Cradle to the Grave", "Pour Out a Little Liquor", "How Long Will They Mourn Me?" na "Str8 Ballin". Mnamo mwaka wa 1996 Big Syke na Shakur walipanga watengeneze toleo la pili la Thug Life: Vol. 2 - Out On Bail ambayo ilitakiwa itolewe na studio ya Makaveli Records, lakini yale mauaji ya mwisho ya mjini Las Vegas yamesababisha hili lisiwe kweli[1]. Japokuwa awali albamu ilitolewa chini ya studio ya Shakur ya Out Da Gutta, Amaru Entertainment, studio ambayo inamilikiwa na mama yake Tupac Shakur, imekuwa ikipata haki zake. Thug Life: Volume 1 ilitunukiwa Dhahabu[2]
Remove ads
Orodha ya Nyimbo
Remove ads
Nafasi ya Chati ya Albamu
Mwaka | Albamu | Nafasi za Chati | |
Billboard 200 | Top Hip Hop Albums | ||
1994 | Thug Life Vol. 1 | #42 | #6 |
Nafasi za Chati za Single
Mwaka | Wimbo | Nafasi ya Chati | |||
The Billboard Hot 100 | Hot R&B/Hip-Hop Singles & Tracks | Hot Rap Singles | |||
1995 | "Cradle to the Grave" | - | #91 | #25 |
Marejeo
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads