Timotheo

From Wikipedia, the free encyclopedia

Timotheo
Remove ads

Timotheo (labda Listra, 17 hivi - Efeso, 97) ni mfuasi mpendwa wa Mtume Paulo, halafu mwandamizi wake [1].

Thumb
Timotheo, mmoja kati ya maaskofu wa kwanza, alivyochorwa katika Nuremberg chronicles f 109v(1493).
Thumb
Picha takatifu ya Kiorthodoksi.

Paulo alimuandikia barua mbili zilizopokewa katika Biblia kati ya Nyaraka za Kichungaji. Habari zake tunazipata humo na katika Matendo ya Mitume.

Tangu kale anaheshimiwa kama askofu mtakatifu na Wakatoliki na Waorthodoksi.

Tangu mwaka 1969, Kanisa Katoliki la Kilatini linamwadhimisha pamoja na Tito tarehe 26 Januari, siku inayofuata ile ya Uongofu wa Mt. Paulo, mwalimu wao.[2][3][4]. Waorthodoksi wanamuadhimisha tarehe 22 Januari.

Remove ads

Tazama pia

Tanbihi

Marejeo ya Kiswahili

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads