Vikta Mauro

From Wikipedia, the free encyclopedia

Vikta Mauro
Remove ads

Vikta Mauro (kwa Kilatini: Victor Maurus) alikuwa askari Mkristo kutoka Mauretania (katika Algeria ya leo).

Thumb
Mozaiki katika kanisa lake mjini Milano.

Mwaka 303 BK, akiwa Milano (nchini Italia), alibomoa altare kadhaa za dini za jadi za Dola la Roma.

Kwa sababu hiyo aliteswa mbele ya Kaizari Maximian na hatimaye kuuawa pamoja na Waberberi wenzake Nabore na Feliche tarehe 12 Julai huko Lodi (Lombardia)[1].

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki, Waorthodoksi na wengineo kama mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 8 Mei[2].

Remove ads

Tazama pia

Tanbihi

Marejeo ya Kiswahili

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads