Visiwa vya Cook

From Wikipedia, the free encyclopedia

Visiwa vya Cook
Remove ads

Visiwa vya Cook (kwa Kiingereza: Cook Islands, kwa Kimaori: Kūki 'Āirani) ni nchi huru ya Polynesia katika Pasifiki iliyopo katika hali ya ushirikiano wa hiari na Nyuzilandi. Mji mkuu wa Avarua uko kwenye kisiwa cha Rarotonga.

Ukweli wa haraka
Remove ads


Thumb
Ramani ya Visiwa vya Cook

Eneo lake ni visiwa vidogo 15 vyenye eneo la km² 240.

Remove ads

Historia

Jina limetolewa kwa kumbukumbu ya mpelelezi Mwingereza James Cook aliyefika kwenye kisiwa cha Manuae mwaka 1773 na kuchora visiwa hivi mara ya kwanza kwenye ramani ya dunia.

Visiwa vilikuwa eneo lindwa la Uingereza katika karne ya 19 kufuatana na ombi la malkia wa Cook aliyeogopa uvamizi wa Ufaransa wakati ule.

Chini ya utawala wa Kiingereza viliwekwa chini ya usimamizi wa serikali ya New Zealand, zikabaki hivyo katika hatua mbalimbali za uhuru wa New Zealand.

Mwaka 1965 New Zealand ikawapa watu wa Cook nafasi ya kujiamulia kuhusu uhuru wao. Visiwa viliamua kujitawala katika ushirikiano na New Zealand. Hatua hiyo ilisimamiwa na Umoja wa Mataifa kwa azimio lake No. 1514 (XV).

Sheria huamuliwa na bunge la visiwa vya Cook. Serikali haisimamiwi na New Zealand. Wananchi wote wana uraia wa New Zealand inayoendesha pia shughuli za jeshi na siasa ya nje kwa niaba ya visiwa. Visiwa vya Cook vimebaki na nafasi ya kufanya mapatano na nchi za nje vilevile.

Remove ads

Demografia

Wakazi ni 15,040 (2021), karibu wote wenye asili ya Kimaori (78.2%) na machotara wa Kimaori (7.6%).[1]

Lugha zinazotumika ni hasa Kiingereza (86.4%) na Kimaori (76.2%).

Upande wa dini, wengi ni Wakristo, hasa Waprotestanti (68.2%) na Wakatoliki (17%).

Uchumi

Utalii ni biashara kuu visiwani.

Picha

Tazama pia

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads