Vita vya Kagera

From Wikipedia, the free encyclopedia

Vita vya Kagera
Remove ads

Vita vya Kagera (kwa Kiingereza: kwa Kiingereza: Uganda-Tanzania War) ni vita vilivyopigwa kati ya Uganda na Tanzania kuanzia tarehe 30 Oktoba 1978 hadi 11 Aprili 1979.

Thumb
Mwalimu Julius Nyerere,1977

Vita hivyo vilihusu kugombania ardhi ya mkoa wa Kagera kati ya nchi ya Tanzania na Uganda.

Katika vita hivyo Tanzania, ikiongozwa na rais Julius Nyerere iliibuka kidedea kwa kuwapiga vema majeshi ya gaidi Idd Amini Dadah yaliyoungwa mkono wa Libya ya Muammar al-Gaddafi na pia Palestina ya Yasser Arafat.

Vita hivyo viliua watu karibu 5,000 na wengine kuachwa yatima.

Remove ads

Historia

Mwanzilishi wa vita hivyo alikuwa Iddi Amini Dadah aliyetaka kupewa na mwl. Nyerere ardhi ya Kagera, tena kwa shuruti ya kivita.

Nyerere aliwaongoza vema wanajeshi 100,000 wa Tanzania akisema, "mchokozi Iddi Amini Dadah ametuchokoza; uwezo wa kumpiga tunao, sababu ya kumpiga tunayo, nia ya kumpiga tunayo, hivyo tumeamua kupambana naye". Aliungwa mkono na Msumbiji na wanaharakati wa Uganda, akiwemo Yoweri Museveni.

Katika vita hiyo Iddi Amini Dadah, baada ya kushambuliwa, alikimbilia nchini Libya, halafu Saudi Arabia hadi mauti yalipompata miaka ya baadaye.

Remove ads

Matokeo

Nchini Uganda ikawa ndiyo mwanzo wa vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Tanzania, iliyolaumiwa na Organization of African Unity kama kwamba ndiyo mvamizi, ililazimika kugharimia peke yake vita na hali ya usalama nchini Uganda baada ya ushindi. Jambo hilo lilizidi kudidimiza nchi katika ufukara na kufelisha mipango yake ya maendeleo. Tanzania ilimaliza kutoka katika hali hiyo mwaka 2007 tu, Uganda ilipolipa madeni yake.

Remove ads

Tanbihi

Marejeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads