Vladimir Mkuu

From Wikipedia, the free encyclopedia

Vladimir Mkuu
Remove ads

Vladimir Mkuu (958 hivi – 15 Julai 1015) alikuwa mtemi wa Kiev na Novgorod kuanzia mwaka 980 hadi kifo chake.

Thumb
Ubatizo wa Vladimir, mchoro wa ukutani wa Viktor Vasnetsov.
Thumb
Ramani inayoonyesha hali ilivyokuwa mwaka 1015 hivi.

Mwaka 988 alipokea ubatizo kutoka kwa mapadre wa Kanisa la Bizanti uliofuatwa na ubatizo wa familia na wananchi wa utemi wake aliojitahidi kwa nguvu zote kuwaleta kwenye imani ya Kikristo [1][2].

Tukio hilo liliathiri moja kwa moja utamaduni wa Urusi, Ukraina na Belarus pamoja na historia yote iliyofuata, kwa kuwa Kanisa la Kiorthodoksi liliendelea kuwa dini rasmi katika milki za Kirusi hadi Mapinduzi ya Urusi ya 1917.

Tangu kale anaheshimiwa na Waorthodoksi na Wakatoliki kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake[3].

Remove ads

Tazama pia

Tanbihi

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads