Volodymyr Zelensky

Rais wa Ukraine. From Wikipedia, the free encyclopedia

Volodymyr Zelensky
Remove ads

Volodymyr Oleksandrovych Zelensky (alizaliwa 25 Januari 1978) ni mwanasiasa, mwandishi na mwigizaji wa filamu, mchekeshaji na rais wa sasa (wa 6) wa Ukraini toka 20 Mei 2019.

Ukweli wa haraka
Remove ads

Utoto na elimu

Volodymyr Zelensky alizaliwa katika familia ya Kiyahudi katika mji wa Kryvyi Rih, wakati ule sehemu ya Jamhuri ya Kisovyeti ya Kijamaa ya Ukraini.[1][2][3][4] Lugha yake ya kwanza ni Kirusi[5].

Baba yake Oleksandr Zelensky alikuwa profesa wa sayansi za kompyuta, mama yake alikuwa mhandisi.[6][7][8] Babu wa Zelensky alikuwa mwanajeshi katika Jeshi Jekundu la Kisovyeti wakazi wa Vita Kuu ya Pili akafikia cheo cha kanali.[9] Ndugu kadhaa wa familia waliuawa na Wajerumani kwa sababu ya kuwa Wayahudi katika Maangamizi Makuu ya Wayahudi.[10] Volodymyr aliendelea kusoma sheria lakini hakufanya kazi ya wakili baada ya kuhitimu.[2]

Remove ads

Mwigizaji na mtayarishaji

Tangu alipokuwa mwanafunzi alitumia nafasi nyingi ya kazi ya mwigizaji. Mwaka 1997 aliunda kundi la waigizaji wachechi la Kvartal 95.[11][12] Kuanzia mwaka 2003 kundi hilo lilitayarisha video kwa ajili ya runinga ya kitaifa ya Ukraini.[13]

Kati ya miaka 2015-2019, Kvartal 95 ilirusha mfululizo wa vipindi vya televisheni vilivyoitwa Servant of the People ambapo Zelensky aliigiza kama Rais wa Ukraini. Chama cha siasa Servant of the People kilianzishwa na wafanyakazi wa Kvartal 95 mnamo Machi 2018.[14][15]

Remove ads

Siasa

Tarehe 31 Desemba 2018, Zelensky alitangaza rasmi kuwa atagombea urais.[16] Miezi sita kabla ya kutangaza nia yake hiyo, alikuwa tayari kati ya wagombea waliokuwa wakiongoza kwenye kura za maoni.[17][15] Zelensky alipata asilimia 30 za kura kwenye awamu ya kwanza ya uchaguzi. Akaingia katika awamu ya pili pamoja na rais mtendaji Petro Poroshenko akashinda kwa kupata asilimia 72.33.[18]

Filamu

Maelezo zaidi Mwaka, Jina ...

Televisheni

Maelezo zaidi Mwaka, Jina ...

Marejeo

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads