Wavaldo

From Wikipedia, the free encyclopedia

Wavaldo
Remove ads

Wavaldo ni Wakristo wafuasi wa Valdo aliyeanzisha tapo la toba ndani ya Kanisa Katoliki mwaka 1173 hivi[1][2][3][4].

Thumb
Nembo ya Wavaldo: Lux lucet in tenebris ("Nuru inang'aa gizani").
Thumb
Sanamu ya Petro Valdo, Worms, Ujerumani.

Hakuna habari nyingi za hakika kuhusu maisha yake. Mfanyabiashara wa Lyon, Ufaransa, aliongoka kwa kuacha mali yake na kushika ufukara.

Alianza pia kuhubiri, hasa kwamba, "Hakuna anayeweza kuyumikia mabwana wawili, Mungu na mali".

Anasifiwa pia kwa kutoa au kuagiza tafsiri ya kwanza ya Biblia katika lugha yoyote mpya iliyotokana na Kilatini.[5]

Mwaka 1179, Valdo na mfuasi wake mmojawapo walikwenda Roma, walipokaribishwa na Papa Alexander III. Mwaka huohuo mtaguso wa tatu wa Laterano ulikataa baadhi ya mawazo ya Valdo, bila kulaani tapo lenyewe wala kutenga na Kanisa viongozi wake.

Lakini itikio la maaskofu lilikuwa kali zaidi, hivyo Wavaldo walifukuzwa kutoka Lyon, na hatimaye walijitafutia usalama katika mabonde ya Piemonte, Italia Kaskazini.[6]

Katika kudai ufukara wa Kiinjili kutoka kwa viongozi wa Kanisa, walikuja kuhukumiwa kama wazushi mwaka 1215 halafu wakadhulumiwa hasa katika karne ya 17.

Katikati (1532) walijiunga na Matengenezo ya Kiprotestanti na kukubali mafundisho ya Yohane Calvin[7].

Kwa sasa wako kama 70,000, hasa Italia Kaskazini.

Remove ads

Tanbihi

Marejeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads