Westside Connection
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Westside Connection ni kundi la muziki wa rap na hip hop kutoka mjini Los Angeles, California, Marekani. Kundi linaongozwa na msanii Ice Cube, WC na Mack 10. Kundi lilitoa albamu yake ya kwanza iliyokwenda kwa jina la Bow Down, na kuweza kushika nafasi ya pili katika chati za Billboard 200 bora za mwaka wa 1996.
Kundi liliazishwa wakati wa kipindi cha mzozo wa wasanii wa hip hop wa East Coast na West Coast, uliozuka baada ya kifo cha marehemu 2Pac. Hawa nao waliwahi kuwa na ugomvi na Cypress Hill, Common, na Q-Tip.
Remove ads
Wasifu
Baada ya kusimama kufanya kazi kwa muda mrefu, kundi likatoa albamu yao ya pili iliyokwendwa kwa jina la Terrorist Threats na ilitoka mnamo mwaka wa 2003, ikiwa imeachiwa na kibado chao mashuhuri cha "Gangsta Nation" kilichomshirikisha rapa Nate Dogg.
Mnamo mwaka wa 2005 Mack 10 aliondoka katika kundi kwa kufuatia kugombana na rapa mwenziwe - WC..[1]
Mnamo mwaka 2008, kulikuwa na fununu zilizoenea kuwa The Game huenda akajiunga na kundi hilo. Uvumi huu unatokana na mistari yake Ice Cube na WC walioimba katika nyimbo ya "Get Used To It" ambamo Game alisema kuwa anaweza kujiunga na Lench Mob (akiwa na maana ya kujiunga na Westside Connection).
Wakati The Game alipoukana uwanachama huo, mda mfupi Ice Cube akiwa katika mahojiano alikiri kuwa mambo hayo yana ukweli ndani yake. Na pale alipoulizwa kuhusu The Game kujiunga na kundi, alijiinamia chini na kusema "labda". [2]
Remove ads
Ugomvi wao na Cypress Hill
Muziki
Albamu zao
Single zao
Marejeo
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads