Wilibrodi

From Wikipedia, the free encyclopedia

Wilibrodi
Remove ads

Wilibrodi (kwa Kiingereza cha Kale: Willibrord; kwa Kilatini: Villibrordus;[1] 658 hivi – 7 Novemba 739) alikuwa mmonaki Mbenedikto kutoka Northumbria (Uingereza) maarufu kama "Mtume wa Wafrisia" kwa uinjilishaji wake katika Uholanzi na Udeni za leo, alipoanzisha majimbo na monasteri mbalimbali[2].

Thumb
Sanamu ya Mt. Wilibrodi huko Echternach.
Thumb
Ukumbusho wa Wilibrodi huko Trier.
Thumb
Kaburi la Mt. Wilibrodi.

Kwa kupewa daraja na Papa Sergio I alikuwa askofu wa kwanza wa Utrecht.

Kisha kuchoshwa na kazi na umri akafariki huko Echternach (leo nchini Luxembourg) katika monasteri mojawapo aliyoianzisha.[3]

Anaheshimiwa tangu zamani na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa katika tarehe ya kifo chake[4].

Remove ads

Tazama pia

Tanbihi

Marejeo ya Kiswahili

Marejeo ya lugha nyingine

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads