Papa Sergio I
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Papa Sergio I alikuwa Papa kuanzia tarehe 15 Desemba 687 hadi kifo chake tarehe 7 Septemba 701[1]. Alitokea Syria[2] au alizaliwa Palermo (Italia) katika familia kutoka Syria[3].

Alimfuata Papa Konon[4][5][5][6][7] akafuatwa na Papa Yohane VI.
Alipigania kwa nguvu zote uinjilishaji wa Wasaksoni na Wafrisia akamfanya mmisionari Wilibrodi kuwa askofu wao.
Pia alimaliza farakano la Akwileia (698)[5] na migogoro mingine, lakini alikuwa tayari kuuawa kuliko kukubali uzushi[8].
Hivyo alikataa kabisa[9][10] kuthibitisha kanuni zilizotungwa na maaskofu wa Mashariki[11] katika Mtaguso wa tano-sita zikilenga kufanya desturi za Konstantinopoli zifuatwe na Wakatoliki wote[12][13]. Kwa sababu hiyo kaisari Justiniani II aliagiza akamatwe na kuletwa Konstantinopoli, lakini watu walizuia utekelezaji wa amri hiyo[5][14].
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu, hasa tarehe 8 Septemba [15].
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Marejeo
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads