Yohane wa Dukla
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Yohane wa Dukla (kwa Kipolandi: Jan z Dukly; Dukla, Polandi, 1414 - Lviv, leo nchini Ukraina, 1484 [1]) alikuwa mtawa na padri wa shirika la Ndugu Wadogo [2]
Maisha
Ingawa alijiunga kwanza na Ndugu Wadogo Wakonventuali, baadaye akahamia urekebisho wa Observansya akaishi maisha ya sala na juhudi za kiroho, lakini pia alifanya kwa ari uchungaji na kulenga umoja wa Wakristo[3].
Hata baada ya kupofuka aliendelea kuandaa hotuba zake maarufu kwa kurudisha watu wengi kwenye Kanisa.[1]
Heshima baada ya kifo
Mara baada ya kifo chake aliheshimiwa kama mtakatifu na miujiza mbalimbali ilisemekana kutokea kaburini pake.
Hatimaye, tarehe 10 Juni 1997, Papa Yohane Paulo II alimtangaza rasmi kuwa mtakatifu katika misa aliyoadhimisha huko Krosno, Poland, wakishiriki watu milioni 1 hivi.
Sikukuu yake ni tarehe 29 Septemba[4].
Tazama pia
Tanbihi
Marejeo
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads