Yosefu Mtungatenzi
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Yosefu mtungatenzi (Sicilia, Italia, 816 - Konstantinopoli, leo nchini Uturuki, 3 Aprili 886) alikuwa mmonaki padri katika monasteri ya Thesalonike, Ugiriki.

Ni maarufu hasa kwa tenzi zake zinazotumika hadi leo hata katika Ukristo wa Magharibi ambazo zimemfanya mmojawapo kati ya watunzi wakuu wa muziki wa Kikristo[1].
Alidhulumiwa sana na serikali kwa kutetea heshima kwa picha takatifu. Kwa ajili hiyo alitumwa pia Roma kuomba ulinzi wa Papa.
Hatimaye alikabidhiwa utunzaji wa vyombo vitakatifu vya kanisa la Hagia Sophia[2].
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu[3].
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Marejeo
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads