Zakaria (Injili)
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Zakaria (kwa Kiebrania זכריה, Zekariah; kwa Kigiriki Ζαχαρίας, Zakarias; kwa Kiarabu زَكَرِيَّا, Zakariya; maana yake ni "YHWH amekumbuka") alikuwa kuhani mwaminifu wa Israeli katika karne ya 1 KK. Mke wake aliitwa Elizabeti, naye pia alikuwa wa ukoo wa Haruni.


Hawakupata mtoto hadi uzeeni kutokana na utasa wa mwanamke, lakini hatimaye walijaliwa kumzaa Yohane Mbatizaji.
Wote wanaheshimiwa kama watakatifu. Sikukuu ya wazazi ni tarehe 5 au 23 Septemba[1], kadiri ya madhehebu. Pengine wanaheshimiwa pamoja na mtoto wao tarehe 24 Juni.
Remove ads
Katika Injili
Habari hizo zinapatikana hasa katika Injili ya Luka, sura ya 1 na ya 2. Humo inaelezwa alivyopashwa na malaika Gabrieli kwamba atapata mtoto wa kiume ambaye atakakuwa nabii mkuu na kumtangulia Bwana[2].
Ingawa Zakaria hakusadiki mara, na kwa sababu hiyo aliadhibiwa kwa kufanywa bubu na kiziwi hadi ahadi itimie, siku ya kumtahiri mtoto alifungua tena kinywa chake kumsifu Mungu Mkombozi na kutoa unabii juu ya ujio wa Kristo, atakayetokea karibuni kutoka juu kama jua linalopambazuka [3].
Kadiri ya Lk 1:68-79, siku hiyo Zakaria alitunga wimbo ambao ni maarufu kwa jina la neno la kwanza katika tafsiri ya Kilatini, Benedictus (yaani "Asifiwe"). Katika madhehebu mbalimbali ya Ukristo, wimbo huo wa Kiinjili unatumika kila siku katika Masifu ya asubuhi.
Remove ads
Katika Kurani
Hata Kurani inamtaja mara kadhaa kama nabii na mzazi wa nabii Yahya, hasa katika sura ya 3 na ya 19.
Tazama pia
Tanbihi
Marejeo ya Kiswahili
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads