Zeila

From Wikipedia, the free encyclopedia

Zeila
Remove ads

Zeila (kwa Kisomali: Saylac, kwa Kiarabu زيلع zayla) ni mji wa bandari wa kihistoria katika mkoa wa magharibi wa Awdal wa Somaliland. [1] Katika Karne za Kati, msafiri Myahudi Benjamini wa Tudela alitambua Zeila (au Hawilah) na eneo la Kibiblia la Havila. [2] Wasomi wengi wa kisasa wanadhani kwamba Zeila ni kati ya miji iliyotajwa katika kitabu cha mwongozo wa biashara kwenye Bahari ya Shamu iliyotungwa kwenye karne ya 2 BK na kuitwa Periplus ya Bahari ya Erythraea. [3] [4]

Thumb
Maghofu ya kihistoria, Zeila
Thumb
Zeila wakati wa usiku

Mji huo uliendelea kuwa kitovu cha awali cha Uislamu. Tangu karne ya 9, Zeila ilikuwa mji mkuu wa Ufalme wa Adal na Usultani wa Ifat katika karne ya 13; na pia mji mkuu wa dola mrithi wake Usultani wa Adal. Wakati wa karne ya 16 iliona kipindi cha ustawi.

Baadaye mji ulikuwa chini ya mamlaka ya Milki ya Osmani na tangu karne ya 18 chini ya Uingereza.

Hadi hivi majuzi Zeila ilikuwa imezungukwa na ukuta mkubwa wenye milango mitano: Bab al Sahil na Bab al-jadd upande wa Kaskazini, Bab Abdulqadir upande wa Mashariki, Bab al-Sahil upande wa magharibi na Bab Ashurbura upande wa kusini. [5]

Zeila iko katika eneo la jadi la ukoo wa kale wa Dir ya Somalia. Mji wa Zeila na wilaya ya Zeila inakaliwa na Wagadabuursi na Waissa, ambao ni koo ndogo za familia ya Dir. [6] [7] [8] [9]

Mazingira ya Zeila ni jangwa. Baharini kuna visiwa vidogo. Mji ulikuwa na vipindi vya ustawi kutokana na biashara yake lakini idadi ya watu ilibaki ndogo kutokana na uhaba wa maji baridi.

Remove ads

Marejeo

Vyanzo

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads