Somaliland

From Wikipedia, the free encyclopedia

Somaliland
Remove ads


Somaliland (kwa Kisomali: Soomaaliland; jina rasmi: Jamhuri ya Somaliland) ni nchi isiyotambuliwa rasmi kimataifa iliyoko katika Pembe ya Afrika. Iko katika pwani ya kusini ya Ghuba ya Aden, ikipakana na Jibuti upande wa kaskazini-magharibi, Ethiopia upande wa kusini na magharibi, na Somalia upande wa mashariki. Eneo linalodaiwa na Somaliland lina ukubwa wa takriban kilomita za mraba 176,120, na lina wakazi wapatao milioni 6.2 kufikia mwaka 2024. Mji mkuu na jiji kubwa zaidi ni Hargeisa.

Ukweli wa haraka

Tangu ilipotangaza kujitenga na Somalia mwaka 1991, Somaliland imekuwa na serikali yake inayojitegemea, taasisi thabiti, bunge, mahakama, jeshi, na sarafu yake, Shilingi ya Somaliland. Ingawa haijatambuliwa rasmi na Umoja wa Mataifa wala nchi nyingi duniani, imekuwa mfano wa utulivu wa kisiasa na utawala wa sheria ikilinganisha na maeneo mengine ya Somalia. Uchumi wake unategemea mifugo, biashara, na uhamishaji wa fedha kutoka kwa raia walioko ughaibuni. Bandari ya Berbera ni lango kuu la biashara, na imekuwa ikiendelezwa kwa ushirikiano na wawekezaji wa kimataifa kama vile DP World.

Kufuatana na mapigano ya Las Anod yaliyotokea mwaka 2022, Somaliland imepoteza sehemu muhimu ya nchi upande wa mashariki kwa wananchi ambao wanapendelea umoja wa kitaifa wakaanzisha utawala wa Khatumo.

Remove ads

Mandhari

Thumb
Mikoa ya Somaliland
Thumb
Somali lahoh (canjeero).
Thumb
Maporomoko ya maji ya Lamadaya kwenye mlima Cal Madow.
Thumb
Eneo la Somaliland.
Thumb
Mandhari ya milima ya Cal Madow, makao ya spishi nyingi za pekee.
Thumb
Ufukwe wa Berbera.
Thumb
Dahabshiil huko Hargeisa.
Thumb
Duka kubwa huko Burao.
Thumb
Hargeisa International Airport huko Hargeisa.
Thumb
Watu mjini Hargeisa.

Historia

Habari za kwanza zinazojulikana kuhusu eneo la Somaliland zasema lilikuwa chini ya milki ya Axum na baadaye Usultani wa Adal.

Bandari ya Berbera ilijulikana tangu zamani za Periplus ya Bahari ya Eritrea.

Katika karne ya 16 Waosmani waliingia wakishika utawala juu ya sehemu za magharibi kwa sababu walitaka kusimamia mlango wa Bahari ya Shamu, Bab el Mandeb.

Walifuatwa na Misri na baadaye Uingereza ambao uliitawala kama "British Somaliland Protectorate" au eneo lindwa la Somalia ya Kiingereza.

Koloni likapewa uhuru wake tarehe 26 Juni 1960 kama Nchi ya Somaliland, ikaungana baada ya siku tano na Somalia ya Kiitalia kuwa Jamhuri ya Somalia.

Wakati wa udikteta wa Siad Barre watu wa kabila la Isaaq waliteswa sana, wakaanza kuchukua silaha dhidi ya rais huyu.

Baada ya kuporomoka kwa serikali yoyote nchini Somalia, wazee wa eneo lililokuwa Somaliland walikutana na kuamua kurudisha uhuru wa awali.

Remove ads

Wakazi

Kuna wakazi milioni 6.2. Zaidi ya nusu ni wafugaji wa kuhamahama na takriban 45 % hukaa mjini au vijijini.

Karibu wote ni Wasomali, hasa wa kabila la Isaaq, wengine ni wa Dir au Darood.

Viungo vya nje

Makala hii kuhusu maeneo ya Somalia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Somaliland kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Remove ads
Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads