From Wikipedia, the free encyclopedia
Ndjamena ni mji mkuu pia mji mkubwa kabisa nchini Chad ikiwa na wakazi 1,093,492 mnamo mwaka 2013.[1]
Jiji la N'Djamena | |
Nchi | Chad |
---|---|
Idadi ya wakazi | |
- Wakazi kwa ujumla | 1,093,492 |
Zamani mji ulijulikana kwa jina la "Fort Lamy". Tangu mwaka 1973 jina limekuwa Ndjamena, N'Djaména, N'Djamena au Ndjaména.
Mji wa Ndjamena uko mahali ambako mito ya Chari na Logone inaungana. Ng'ambo ya mto uko mji wa Kousseri nchini Kamerun.
Ndjamena ilianzishwa na Mfaransa Émile Gentil tarehe 29 Mei 1900 kama kambi ya kijeshi ikiitwa Fort-Lamy kama kumbukumbu ya kamanda Amédée-François Lamy aliyeuawa vitani kwenye mapigano ya Kousseri siku chache kabla ya kuanzishwa kwa Fort Lamy[2][3] .
Jina lilibadilishwa na rais François Tombalbaye kuwa Ndjamena mwaka 1973. Wakati wa vita ya wenyewe kwa wenyewe ya Chad 1979 / 1980 mji uliharibika na wakazi wengi waliondoka mjini lakini katika miaka ya baadaye wengine wengi waliingia.[4]
Mji ulikua sana na haraka. Huduma za maji, umeme na makao havitoshi tena.
Mwaka * Idadi ya Wakazi
Makabila na vikundi mjini mwaka 1993:
Ndjamena ina vyuo na shule mbalimbali kama vile.
Shule za Sekondari (Lycée) :
Vyuo Vikuu (Université) :
Taasisi za elimu ya juu (École Supérieure) :
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.