From Wikipedia, the free encyclopedia
Watakatifu wote (kwa Kigiriki: Αγίων Πάντων, Agiōn Pantōn) ni sherehe ya liturujia katika madhehebu mengi ya Ukristo[1][2][3][4][5] inayoadhimishwa tarehe 1 Novemba katika Kanisa la Kilatini[6] na madhehebu kadhaa ya Uprotestanti.
Desturi hiyo ya Ukristo wa magharibi inatokana na kwamba katika mwaka wa Kanisa mwezi Novemba ni wa mwisho, hivyo umeonekana unafaa kuutumia kutafakari juu ya mambo ya mwisho: kifo, hukumu, moto na mbingu. Watakatifu ni watu wanaosadikiwa wamekwishaingia huko Paradiso walau kwa roho yao, kama mhalifu aliyetubu karibu na Yesu msalabani.
Kumbe katika Ukristo wa mashariki huadhimishwa Jumapili ya kwanza baada ya Pentekoste, ili kusisitiza uhusiano wa utakatifu wa binadamu na Roho Mtakatifu. Ni yeye tu anayewawezesha kushinda dhambi katika maisha yao.
Walengwa wa heshima hiyo, baada ya Mungu aliyewatakasa kwa njia ya Yesu Kristo, ni watakatifu wote, wanaojulikana na wasiojulikana sawia.
Ingawa kila mtakatifu anakumbukwa siku maalumu ya mwaka, sikukuu hii ya pamoja inasisitiza uzuri wa umoja wao mbinguni, pamoja na wingi wao, kama ulivyosisitizwa na Mtume Yohane katika kitabu cha Ufunuo. Hivyo ni chanzo cha tumaini jipya kwa binadamu wanaosafiri bado duniani kuelekea huko kati ya majaribu mengi.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.