Adalbert wa Magdeburg
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Adalbert wa Magdeburg (alifariki 20 Juni, 981) alikuwa mmisionari na askofu mkuu wa kwanza wa mji wa Magdeburg, Ujerumani.

Tangu kale ametambuliwa kuwa mtakatifu.
Maisha
Adalbert alizaliwa Ujerumani na kuwa mtawa katika monasteri ya Wabenedikto wa mji wa Trier.
Baada ya kuwekwa wakfu kama askofu, mwaka 961 alitumwa mjini Kiev (Ukraine) kama mmisionari.
Kundi lake lote liliuawa, naye peke yake aliweza kurudi Ujerumani.
Baadaye aliteuliwa kuwa askofu mkuu wa dayosisi ya Magdeburg.
Alianzisha madayosisi mapya mengi upande wa Mashariki wa Ujerumani, kama katika miji ya Naumburg, Meisen, Merseburg, Brandenburg, Havelberg, na Poznan.
Mwanafunzi wake mmoja aliyetangazwa kuwa mtakatifu kama yeye ni Adalbert wa Praha.
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Marejeo ya Kiswahili
Marejeo ya lugha nyingine
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads