Adalbert wa Prague
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Adalbert wa Prague (kwa Kicheki Vojtěch, kwa Kipolandi Wojciech, kwa Kijerumani Adalbert, jina alilojichagulia alipopewa Kipaimara na Adalbert wa Magdeburg ; Libice, leo nchini Ucheki 956 hivi – Tenkitten, leo nchini Urusi, 23 Aprili 997) alikuwa askofu wa Prague (Ucheki) tangu mwaka 983.



Huko alipatwa na matatizo mengi akafanya safari nyingi kwa jina la Kristo, akijitahidi kwa nguvu zote kung'oa desturi za Kipagani. Alipotambua kwamba matunda yake ni machache, alikwenda Roma akawa mmonaki Mbenedikto.
Hatimaye alikwenda Polandi ili kuwaletea imani Waprusia, akachomwa kwa mikuki na Wapagani kadhaa[1].
Mwaka 999 alitangazwa na Papa Silvesta II kuwa mtakatifu mfiadini.
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Marejeo
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads