Ana Schaeffer
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Ana Schaeffer (Mindelstetten, Bavaria, Ujerumani, 18 Februari 1882 – Mindelstetten, 5 Oktoba 1925), alikuwa mwanamke mwenye karama za pekee katika maisha ya ugonjwa[1] nyumbani akizama katika sala.

Ni kwamba, alipokuwa na umri wa miaka 19, akiwa mfanyakazi wa ndani, alimwagikiwa maji ya moto, tukio lililozidi kuathiri vibaya afya yake; hata hivyo aliishi kwa utulivu katika ufukara, akimtolea Mungu msalaba wa maumivu yake kwa ajili ya wokovu wa watu[2].
Mwaka 1910 alijikuta ana madonda mwilini kama yale ya Yesu msulubiwa[3]. Pia alipata njozi.
Alitangazwa na Papa Yohane Paulo II kuwa mwenye heri tarehe 7 Machi 1999[4], halafu Papa Benedikto XVI alimtangaza mtakatifu tarehe 21 Oktoba 2012[5].
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads