Ansgar Mtakatifu
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Mtakatifu Ansgar (Amiens, Ufaransa, labda 8 Septemba 801 – Bremen, Ujerumani, 3 Februari 865) alikuwa askofu mmisionari huko Skandinavia.

Tangu kale ametambuliwa kuwa mtakatifu.
Sikukuu yake ni 3 Februari[1].
Maisha
Ansgar alijiunga na monasteri huko Corbie.
Mwaka 826 alikwenda kuhubiri Injili nchini Denmark, ambako hakufanikisha sana, hivyo akaenda Uswidi.
Alikuwa askofu wa Hamburg, halafu akaongezewa Bremen pia, upande wa kaskazini wa Ujerumani. Ndipo alipofariki kutokana na uchovu wa kazi zake, Pia alikuwa balozi wa Papa Gregori IV katika Denmark na Uswidi[2].
Alivumilia magumu mengi sana katika kazi ya uenezaji Injili, asikate tamaa.
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Marejeo ya Kiswahili
Marejeo ya lugha nyingine
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads