Bujora
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Bujora ni kata iliyopo katika Wilaya ya Magu, Mkoa wa Mwanza nchini Tanzania iliyopata umaarufu kutokana na hifadhi ya utamaduni wa kabila la Wasukuma.
Makumbusho ya Wasukuma yalianzishwa rasmi mwaka 1968[1] kwa ajili ya kuendeleza na kutunza utamaduni na mila za kabila la Wasukuma [2]
Msingi wa hifadhi ya Bujora uliwekwa katika miaka ya 1950 na Padri David Clement wa shirika la Wamisionari wa Afrika (White Fathers) kutoka nchini Kanada. Malengo yake yalikuwa kuunganisha utamaduni wa Kisukuma na Ukristo, maarufu kama utamadunisho (kwa Kiingereza "inculturation").[3][4]
Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi wa kata walihesabiwa kuwa 31,787 [5].
Remove ads
Marejeo
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads