Ukiki

Ndege wakubwa kiasi wa jenasi Ceuthmochares, familia Cuculidae From Wikipedia, the free encyclopedia

Ukiki
Remove ads

Ukiki au pundamakaa ni ndege wakubwa kiasi wa jenasi Ceuthmochares katika nusufamilia Phaenicophaeinae ya familia Cuculidae wanaofanana na kekeo. Wana mnasaba na malkoha wa Asia. Wanatokea misitu wa Afrika kusini kwa Sahara. Rangi yao ni buluu au kijani na wana domo njano (kwa sababu ya hii huitwa yellowbill kwa Kiingereza). Hula wadudu wakubwa hasa lakini konokono, vertebrata wadogo, matunda na mbegu pia. Kinyume na kekeo hutengeneza tago lao lenyewe katika mti. Jike hutaga mayai meupe mawili.

Maelezo zaidi Uainishaji wa kisayansi, Ngazi za chini ...
Remove ads

Spishi

Picha

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads