Chata

From Wikipedia, the free encyclopedia

Chata
Remove ads

Chata ni nyoka wasio na sumu wa jenasi Boaedon na Lamprophis katika familia Lamprophiidae.

Maelezo zaidi Uainishaji wa kisayansi, Ngazi za chini ...

Nyoka hawa ni warefu kiasi, sm 150 kwa kipeo lakini kwa wastani majike ni sm 60-100 na madume sm 40-70. Wana mkia mrefu kiasi, kichwa kwa umbo wa pembetatu na mboni za wima. Rangi yao ni kahawia, kahawianyekundu, kijivu au nyeusi. Kuna milia miwili myeupe pande mbili za kichwa na milia hii inaweza kuendelea mpaka mkia.

Chata hupumzika mchana katika vishimo au chini ya miamba, magogo au takataka. Huwinda usiku na hukamata panya hasa lakini ndege, mijusi na vyura pia. Waama, nyoka hawa ni muhimu sana kwa sababu wanasaidia watu kwa kuwaua wagugunaji wengi.

Nyoka hawa hawana sumu lakini spishi kadhaa hung'ata na kusababisha vidonda. Kwa kawaida huwa wanyama-vipenzi katika muda mfupi.

Remove ads

Spishi

Remove ads

Picha

Marejeo

  • Spawls, S., Howell, K., Drewes, R. & Ashe, J. (2002) A field guide to the Reptiles of East Africa. Academic Press, San Diego, CA, USA.

Viungo vya nje

Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Chata kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads