Chipsi

From Wikipedia, the free encyclopedia

Chipsi
Remove ads

Chipsi (kutoka Kiingereza: "chips"; pia: vibendo, viepe) ni vipande vyembamba vya chakula vilivyokaangwa katika mafuta. Kwa kawaida huongezewa chumvi na mayai au kitoweo kingine.

Thumb
Chipsi moto au vibanzi
Thumb
Chipsi baridi.
Thumb
Chiipsi za tortilla.

Aina

Chipsi zinajulikana hasa kama chipsi za viazi, tena kwa namna mbili tofauti:

  • Chipsi baridi (kwa Kiingereza: potato chips, crisps) ni vipande bapa na vyembamba sana vya chipsi ambavyo vinakaangwa katika mafuta hadi kukauka kabisa. Chipsi hizo huliwa mara nyingi peke yake. Vinauzwa madukani katika mfuko na kuliwa kama chakula baridi. Chipsi baridi hutengenezwa pia kwa kutumia ndizi, mizizi mingine yenye wanga au nafaka mbalimbali.
Remove ads

Chipsi na afya

Chipsi za kila aina ni chakula kinachopendwa lakini kina pia madhara ya kiafya. Chipsi mara nyingi zina kiwango kikubwa cha mafuta na hivyo zinachangia kutokea kwa unene wa kupindukia. Pia zinatayarishwa na chumvi na mlaji anapita haraka kiasi cha chumvi kinacholingana na afya (gramu 6/siku kwa mtu mzima).

Kama chipsi zimekaangwa katika mafuta yasiyo mapya au kwa joto kubwa mno kuna kemikali zinazoweza kusababisha kansa.

Remove ads

Angalia pia

Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Chipsi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads