Köln

From Wikipedia, the free encyclopedia

Köln
Remove ads

Köln (pia: Kolon, kutokana na Kifaransa Cologne; kwa Kijerumani cha kienyeji: Kölle) ni mji wa Ujerumani kando ya mto Rhine wenye wakazi 970,000.

Ukweli wa haraka Nchi, Jimbo ...
Thumb
Mji wa Köln
Thumb
Kölner Seilbahn na Mghorofa wa AXA (nyuma)
Thumb
Köln Zoo
Thumb
Makumbusho ya Romania/Germania (Kati), makumbusho Ludwig (kulia), kanisa kuu (kushoto)
Thumb
Ziwa la Aachen Köln
Thumb
Soko la krismasi huko Mülheimplatz
Thumb
Mnara wa radio Colonius' kushoto: magorofa ya Herkules (rangi nyekundu/bluu), bustani mkanda kijani (kulia)
Daraja la kusini Köln
Remove ads

Historia

Maana asili ya jina ni "koloni". Ni mji wa kale ulioundwa kwa jina la "Colonia Claudia Ara Agrippinensis" kama koloni ya Waroma wa Kale mnamo mwaka 50. Mahali pa mji paliwahi kuwa boma la Kiroma na kabla ya hapo kijiji cha kabila cha Waubii.

Köln ni mji mkubwa wa nne wa Ujerumani na mji mkubwa wa jimbo la Rhine Kaskazini - Westfalia (Nordrhein-Westfalen).

Kuna kanisa kubwa kuliko yote ya Ujerumani ("Kölner Dom") ambalo ni maarufu kwa sababu limejengwa katika muda wa miaka 700 tangu mwaka 1248 hadi 1880. Masalia ya mamajusi watatu waliomtembelea mtoto Yesu huko Bethlehemu yanasemekana kutunzwa humo. Köln ni kitovu muhimu wa Kanisa Katoliki nchini na makao wa askofu mkuu.

Chuo kikuu chake kilianzishwa mwaka 1388 na leo kuna wanafunzi 44,000 na pamoja na vyuo vingine kuna wanafunzi zaidi ya 80,000 kwenye ngazi ya vyuo. Kati ya vyuo vingine Chuo cha Muziki kimejulikana sana kimataifa.

Spa ya Neptun na Claudius Isotherm ni spa kubwa huko Köln.

Mji umejulikana pia kwa aina yake ya pekee ya bia.

Köln ni pia kitovu cha Waafrika katika Ujerumani. Pamoja na wanafunzi wengi kutoka Afrika kuna pia taasisi kama huduma ya Sauti ya Ujerumani (Deutsche Welle) zinazoajiri Waafrika wengi. Kuna hata vilabu ambako bia aina ya Tusker kutoka Kenya inauzwa.

Mwaka 2005 Köln ilikuwa mahali pa Siku ya kimataifa ya vijana Wakatoliki; zaidi ya milioni moja walikutana na Papa Benedikto XVI.

Watalii wengi wanafika kila mwaka kwa sherehe ya Karnivali kabla ya majira ya Kwaresima.

Remove ads

Picha

Trafiki

Thumb
Kituo cha Köln Messe / Deutz
Thumb
Kituo cha treni za mji Köln Piusstrasse
Thumb
Kituo cha reli Köln West

Kuna usafiri wa umma wa Treni za mji Köln (Stadtbahn), Treni za mkoa Rhein / Sieg reni za mkoani (S-Bahn), treni za eneo (RB, RE) na mabasi la mji na mabasi la eneo.

Huduma za treni za masafa marefu ipo Kituo kikuu cha reli Köln, kituoni cha Messe/Deutz na kituoni cha reli ya uwanja wa ndege Köln/Bonn, kwenye kituo cha uwanja wa ndege kuna kituo cha basi la masafa marefu pia.

Tazama pia

Viungo vya nje

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu maeneo ya Ujerumani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Köln kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Remove ads
Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads