Daniel Comboni
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Daniele Comboni (Limone sul Garda, Italia 15 Machi 1831 - Khartoum, Sudan, 10 Oktoba 1881), alikuwa askofu mmisionari wa Kanisa Katoliki nchini Sudan, akijitosa bila kujibakiza katika kuhubiri Injili na kuhudumia kwa kila namna heshima ya binadamu wa maeneo yale [1].
Ndiye aliyeanzisha mashirika ya Wamisionari wa Moyo Mtakatifu wa Yesu na Masista wa Afrika, wanaojulikana kama Wamisionari Wakomboni na Masista Wakomboni.
Alitangazwa na Papa Yohane Paulo II kuwa mtakatifu tarehe 5 Oktoba 2003.
Remove ads
Maisha
Daniele Comboni alikuwa moja kati ya ndugu wanane, lakini ndugu zake walifariki wote walipokuwa watoto.
Daniele aliacha wazazi wake alipokuwa na miaka 12 na alienda Verona kusoma kwenye shule ya padri Nicola Mazza ambapo alichagua kuwa padri na kwenda Afrika kama mmisionari.
Alifika Misri na wamisionari wengine watano (1857). Wote waliendelea hadi kufika Sudan kusini.
Baada ya miaka miwili Daniele alirudi Italia kwa sababu wamisionari wenzake walifariki huko Sudan.
Siku moja, alipokuwa akiomba ndani ya basilika la Mt. Petro mjini Roma alitafakari kuhusu njia ya kueneza Injili barani Afrika.
Aliandika “Mpango ya Kuirudishia Afrika Uhai”. Katika mpango huu Comboni alisema ya kwamba ni lazima kusaidia Waafrika kukua katika elimu ili wenyewe waweze kupanga maendeleo yao.
Mwaka 1867 alianza shirika la mapadre na mabruda.
Mwaka 1877 alipewa na Papa daraja takatifu ya askofu ili kujenga Kanisa katika Afrika ya Kati (Sudan, Sudan Kusini, Uganda, Kenya ya leo).
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Marejeo ya Kiswahili
Marejeo ya lugha nyingine
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads