Daudi Lewis
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Daudi Lewis, S.J. (Abergavenny, Monmouthshire, Welisi, 1616 - Usk 27 Agosti 1679), alikuwa padri Mjesuiti aliyefanya uchungaji kwa siri muda wa miaka 30 huko Welisi (Ufalme wa Muungano)[1].

Mtoto wa kasisi wa Jumuiya Anglikana, aliongokea Kanisa Katoliki huko Paris (Ufaransa) akasomea upadri huko Roma (Italia). Miaka mitatu baada ya kupadrishwa mwaka 1642 alijiunga na Shirika la Yesu.
Hatimaye alifia imani yake kutokana na dhuluma ya mfalme Charles II[2].
Anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu mfiadini. Kwanza alitangazwa mwenye heri na Papa Pius XI mwaka 1929, halafu mtakatifu na Papa Paulo VI tarehe 25 Oktoba 1970.
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Vyanzo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads