Dedan Kimathi
Kiongozi wa Kenya katika kuchipuka kwa Mau Mau (1920-1957) From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Dedan Kìmathi Waciūri (alizaliwa kama Kìmathi Waciūri) tarehe 31 Oktoba 1920 – 18 Februari 1957) alikuwa kiongozi wa Kenya Land and Freedom Army wakati wa Mau Mau Uprising (1952-1960) dhidi ya utawala wa Kikoloni wa Waingereza nchini Kenya katika miaka ya 1950.Alikamatwa na Waingereza mwaka wa 1956 na kuhukumiwa kifo mwaka wa 1957.Kenya ilipata uhuru mwaka wa 1963.[1]Kìmathi anasifiwa kwa kuongoza juhudi za kuunda miundo rasmi ya kijeshi ndani ya harakati za Mau Mau,na kuitisha baraza la vita mwaka wa 1953. Yeye pamoja na Baimungi M'marete,Musa Mwariama,Kubu Kubu,General China na Muthoni Kirima ambaye alikuwa mmoja wa Majemedari Wakuu.
Kwa maana nyingine, tazama Dedan Kimathi (kata).

Wakenya wanamtambua kama mpigania uhuru katika harakati za Kenya za kupigania uhuru, ilhali mamlaka za kikoloni za Kiingereza zilimwita Kìmathi gaidi na kulingana na mwanahistoria David Anderson,"did all they could to besmirch his reputation."Licha ya kuonekana kwa mtazamo hasi na marais wawili wa kwanza wa Kenya,Jomo Kenyatta na Daniel Arap Moi,Kìmathi na waasi wenzake wa Mau Mau walitambuliwa rasmi kama mashujaa katika harakati za kupigania uhuru wa Kenya chini ya utawala wa Mwai Kibaki hatua iliyohitimishwa na ufunguzi wa sanamu ya Kìmathi mwaka wa 2007.Hili liliimarishwa zaidi na kupitishwa kwa Katiba mpya mwaka wa 2010, iliyotaka kutambuliwa kwa mashujaa wa taifa.
Remove ads
Maisha ya mwanzo
Kìmathi huenda alizaliwa takribani mwaka wa 1920 katika Kaunti ya Nyeri ya leo, ambako baba yake, aliyethamini elimu, alimpeleka shuleni.Kìmathi alifanya vyema shuleni, na ujuzi wake wa kuandika na kuzungumza ulitambulika.Hata hivyo, Anderson anaandika kwamba Kìmathi alikuwa na roho ya ushindani mkubwa, alikuwa akiwatisha wenzake, na mara kwa mara alichukuliwa hatua za kinidhamu na walimu.Kìmathi alisafiri kuenda Nairobi mwishoni mwa miaka ya 1930 na kujiunga na jeshi la Waingereza mwaka wa 1940, lakini, kulingana na Anderson, alifukuzwa jeshini baada ya mwezi mmoja, ikidaiwa ni kwa sababu ya ulevi na vurugu. Baada ya hapo, alihama kutoka kazi moja hadi nyingine kuanzia kuchunga nguruwe hadi kuwa mwalimu wa shule ya msingi ambako aliripotiwa kufutwa kazi baada ya kushutumiwa kwa kutumia vurugu dhidi ya wanafunzi wake.
Remove ads
Harakati ya Mau Mau
Takriban mwaka wa 1947 au 1948, wakati akifanya kazi Ol Kalou, Kìmathi alikutana na wanachama wa Kenya African Union (KAU).Kufikia mwaka wa 1950, alikuwa amekuwa katibu wa tawi la KAU katika Ol Kalou, ambalo lilikuwa chini ya udhibiti wa wafuasi wakali wa harakati ya Mau Mau.Mau Mau ilianza kama Kenya Land and Freedom Army(KLFA), jeshi la wapiganaji kutoka jamii za Kikuyu,Embuna Merulililolenga kurejesha ardhi ambayo wakoloni Waingereza walikuwa wamewapokonya polepole.Kadiri ushawishi na uanachama wa kundi hilo ulivyoongezeka, likawa tishio kubwa kwa serikali ya kikoloni.
Baada ya kula kiapo cha Mau Mau, Kìmathi alijiunga na Forty Group mwaka wa 1951, ambacho kilikuwa tawi la wapiganaji la chama kilichokuwa kimevunjika cha Kikuyu Central Association.Kama katibu wa tawi, Kìmathi aliendesha shughuli za kula viapo. Alikuwa na imani kwamba kuwalazimisha Wakikuyu wenzake kuapa kungeleta umoja katika harakati za kupigania uhuru. Ili kufanikisha hilo, aliwapa watu adhabu za viboko na kubeba bunduki ya mapacha.Shughuli zake ndani ya kundi hilo zilimfanya kuwa shabaha ya serikali ya kikoloni, na alikamatwa kwa muda mfupi mwaka huo huo lakini akatoroka kwa msaada wa askari wa eneo hilo. Tukio hilo lilianza ushiriki wake rasmi katika mapambano ya Mau Mau, na mwaka wa 1953 alianzisha Kenya Defence Council ili kuratibu wapiganaji wote wa msituni.
Remove ads
Kukamatwa na Kuuawa
Mapambano ya Kìmathi kwa ajili ya uhuru wa Kenya yalifikia kikomo mwaka wa 1956.Tarehe 21 Oktoba mwaka huo,Ian Henderson afisa wa polisi wa kikoloni wa Uingereza ambaye alikuwa katika "obsessive hunt" kumtafuta Kìmathi, aliweza kumnasa katika maficho yake msituni.Kìmathi alipigwa risasi mguuni na kukamatwa na askari wa kabila (Tribal Policeman) aliyeitwa Ndirangu Mau, ambaye alimpata Kìmathi akiwa na panga. Kukamatwa kwake kulikuwa ishara ya mwisho wa vita vya msituni; picha ya Kìmathi akiwa amebebwa kwenye machela ilichapishwa kwenye vipeperushi (takriban 120,000 vilisambazwa) na Waingereza ili kuwavunja moyo wapiganaji wa Mau Mau na wafuasi wao. Kìmathi alishtakiwa kwa kosa la kumiliki bastola aina ya .38 Webley Scott.
Mahakama iliyokuwa ikiongozwa na Jaji Mkuu O'Connor pamoja na washauri watatu Waafrika ilimhukumu kifo Kìmathi wakati alipokuwa amelazwa katika Hospitali Kuu ya Nyeri. Rufaa yake ilikataliwa, na hukumu ya kifo ikaendelea kutekelezwa.
Siku moja kabla ya kunyongwa, aliandika barua kwa Padre Marino akimwomba amsaidie mwanawe kupata elimu:"He is far from many of your schools, but I trust that something must be done to see that he starts earlier under your care."Pia aliandika kuhusu mke wake, Mūkami, akisema: "She is detained at Kamìtì Prison and I suggest that she will be released some time. I would like her to be comforted by sisters e.g. Sister Modester, etc. for she too feels lonely. And if by any possibility she can be near the mission as near Mathari so that she may be so close to the sisters and to the church."
Aliomba kumuona mke wake, na asubuhi ya siku ya kunyongwa Mūkami aliruhusiwa kumuona katika Gereza la Kamìtì. Wawili hao walizungumza kwa takriban saa mbili. Alimwambia kwamba "I have no doubt in my mind that the British are determined to execute me. I have committed no crime. My only crime is that I am a Kenyan revolutionary who led a liberation army... Now If I must leave you and my family I have nothing to regret about. My blood will water the tree of Independence."
Asubuhi ya mapema tarehe 18 Februari 1957, alinyongwa katika Kamiti Maximum Security Prison Alizikwa kwenye kaburi lisilo na alama, na mahali alipozikwa palibaki kuwa siri kwa miaka 62 hadi tarehe 25 Oktoba 2019, ambapo Taasisi ya Dedan Kìmathi iliripoti kuwa kaburi lake lilikuwa limepatikana katika eneo la gereza la Kamìtì.
Remove ads
Maisha binafsi
Kìmathi alikuwa amemuoa Mūkami Kìmathi. Miongoni mwa watoto wao ni wavulana Waciūrì na Maina, na wasichana Nyambura, Waceke, Wangeci, Nyakìnyua Nyawìra, Mūthoni, Wangūi na Wanjūgū. Serikali ilimjengea Mūkami nyumba yenye vyumba vitatu katika shamba lake lililoko Kinangop, Kaunti ya Nyandarua mwaka wa 2009, na mwaka wa 2012 likampatia gari aina ya double cabin pickup kwa matumizi binafsi. Mwaka 2010, mjane wa Kìmathi aliomba uchunguzi wa kutafuta mwili wa mumewe uanze upya ili aweze kumzika kwa heshima. Mūkami Kìmathi alifariki dunia tarehe 4 au 5 Mei 2023 na alizikwa Njabini, Kinangop.
Remove ads
Urithi
Usajili rasmi wa Mau Mau
Tarehe 11 Novemba 2003, serikali ya Kibaki ilisajili rasmi harakati za Mau Mau, ikipuuzilia mbali sheria za enzi za ukoloni zilizokuwa zimepiga marufuku shirika hilo na kuwaita wanachama wake “magaidi.” Katika hotuba yake wakati wa kukabidhi cheti cha usajili, Makamu wa Rais Moody Awori alieleza masikitiko yake kwamba ilichukua miaka 40 kwa kundi hilo kusajiliwa rasmi licha ya kujitolea kwao kupigania uhuru wa Kenya.
Sanamu ya Dedan Kìmathi
Serikali ya Kibaki ilijenga sanamu ya shaba yenye urefu wa mita 2.1 iliyopewa jina Freedom Fighter Dedan Kimathi juu ya msingi wa granite katikati mwa jiji la Nairobi. Sanamu hiyo ipo katika makutano ya Barabara ya Kimathi na Barabara ya Mama Ngina. Kìmathi, akiwa amevalia mavazi ya kijeshi,ana bunduki mkononi wa kulia na kisu mkononi wa kushoto silaha alizotumia katika mapambano yake ya mwisho. Jiwe la msingi la sanamu hiyo liliwekwa na Makamu wa Rais Moody Awori tarehe 11 Desemba 2006, na sanamu hiyo ilizinduliwa rasmi na Rais Mwai Kibaki tarehe 18 Februari 2007, ikiambatana na kumbukumbu ya miaka 50 tangu aliponyongwa. Katika hotuba yake, Kibaki alimpongeza Kìmathi kama mtu ambaye si tu alijitoa mhanga kwa ajili ya ukombozi wa Kenya bali pia aliwapa wengine motisha ya kupigania uhuru dhidi ya ukandamizaji.
Sanamu hiyo ilipokelewa kwa pongezi nyingi kutoka kwa Wakenya kama ishara iliyocheleweshwa kwa muda mrefu ya kutambua mchango wa wapiganaji wa Mau Mau katika harakati za kupigania uhuru. Hili lilikuwa tofauti kabisa na mtazamo wa serikali za baada ya ukoloni za Jomo Kenyatta na Daniel Arap Moi, ambazo zilikuwa zikiwachukulia wanaharakati wa Mau Mau kama magaidi.
Tarehe 12 Septemba 2015, serikali ya Uingereza ilizindua sanamu ya kumbukumbu ya Mau Mau katika Uhuru Park, Nairobi, ambayo iliifadhili, “kama ishara ya upatanisho kati ya serikali ya Uingereza, Mau Mau, na wote waliokumbwa na mateso.” Hii ilifuatia uamuzi wa Uingereza mwezi Juni 2013 wa kulipa fidia Wakenya zaidi ya 5,000 waliotendewa mateso na ukatili wakati wa mapambano ya Mau Mau.
Nelson Mandela
Kìmathi aliheshimiwa sana na kiongozi wa kupigania kuondolewa kwa ubaguzi wa rangi (apartheid )Nelson Mandela.Mwezi Julai 1990, miezi mitano baada ya kuachiliwa huru kutoka kifungo cha miaka 27 alichokibebwa chini ya utawala wa ubaguzi wa rangi wa Afrika Kusini, Mandela alitembelea Nairobi na kuomba kuliona kaburi la Kìmathi na pia kukutana na mjane wake, Mūkami.Ombi la Mandela lilikuwa wakati wa aibu kwa utawala wa Moi, ambao kwa kiasi kikubwa ulikuwa umemsahau Kìmathi kama ilivyokuwa kwa serikali ya Jomo Kenyatta kabla yake. Kulikuwa ni wakati wa kutilia shaka akijaribu kumtafuta Mūkami katika kijiji ambacho yeye na familia yake walikuwa wamesahaulika katika umasikini. Ombi la Mandela halikukubalika. Wakati wa hotuba yake ya umma katika Uwanja wa Kasarani, Nairobi, kabla ya kuondoka nchini, Mandela alieleza heshima yake kwa Kìmathi, Musa Mwariama, Waruhiu Itote, Kubu Kubu na viongozi wengine wa Mau Mau waliomvutia katika mapambano yake dhidi ya ukatili. Ilikuwa miaka 15 baadaye tu, mwaka 2005, wakati wa ziara yake ya pili nchini Kenya, ambapo Mandela hatimaye aliweza kukutana na Mūkami pamoja na watoto wawili wa Kìmathi.
Heshima ya Mandela kwa Kìmathi tayari mwanzoni mwa miaka ya 1960 pia inatajwa katika kitabu My Moment with a Legend cha Ronnie Kasrils, mkuu wa zamani wa uchunguzi wa tawi la kijeshi la ANC, Umkhonto We Sizwe (MK), na waziri wa ulinzi katika serikali ya Mandela.
Maeneo yaliyopewa jina la Kìmathi
- Dedan Kìmathi University of Technology (Nyeri Country)
- Dedan Kìmathi Stadium, Nyeri, Kenya (formerly known as Kamukunji Grounds)
- Kìmathi Street, Nairobi, Kenya – One of the main roads in Nairobi's Central Business District and where there is a statue in his honor
- Dedan Kìmathi Road, Lusaka, Zambia - Situated on this road is the Intercity Bus Terminus and ZCAS University.
- Kìmathi Avenue, Kampala, Uganda
- Dedan Kìmathi Road, Mombasa, Kenya
- Kìmathi Road, Nyeri Town, Kenya
- Kìmathi Road, Nanyuki Town, Kenya
- Dedan Kìmathi Street, Embalenhle, Mpumalanga, South Africa
- Dedan Kìmathi Memorial High School, Nyeri, Kenya
- Kìmathi Crescent, Isamilo, Mwanza, Tanzania
Utamaduni maarufu na kusoma zaidi
- The Trial of Dedan Kìmathi (play) – Micere Mugo and Ngũgĩ wa Thiong'o
- Karimi, Joseph (2013). Dedan Kimathi: The Whole Story. Jomo Kenyatta Foundation.
- Mukami Kìmathi (2017). Mau Mau Freedom Fighter. Mdahalo Bridging Divides Limited.
- Henderson, Ian; Philip Goodhart (1958). The Hunt for Kimathi. London: Hamish Hamilton. OCLC: 272575
- Kahiga, Samuel (1990). Dedan Kimathi: The Real Story.
- Maina wa Kinyatti. Kenya's Freedom Struggle: The Dedan Kimathi Papers.
- Jabali Afrika (2011). Dedan Kìmathi (song)
Remove ads
Marejeleo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads
