Batamiti

From Wikipedia, the free encyclopedia

Batamiti
Remove ads

Mabatamiti au Dendrocygninae ni nusufamilia ya familia ya Anatidae yenye jenasi moja tu, Dendrocygna. Waainishaji wengine wanawaweka ndani ya familia yao wenyewe Dendrocygnidae au ndani ya kabila Dendrocygnini ya familia ndogo Anserinae. Leo kuna spishi nane za mabatamiti na visukuku vya spishi ingine vimefunuliwa kisiwani kwa Aitutaki, Visiwa vya Cook. Wanaitwa mabatamiti kwa sababu hujenga matago yao pengine ndani ya miti. Lakini kwa Kiingereza wanaitwa “whistling ducks” sikuhizi kwa sababu ya sauti yao kama mluzi. Mabata hawa wanatokea popote kwa kanda za tropiki na nusutropiki. Wana miguu mirefu na shingo refu na wanapenda kuwa pamoja. Makundi makubwa ya ndege hawa huonekana maziwani.

Maelezo zaidi Uainishaji wa kisayansi, Ngazi za chini ...
Remove ads

Spishi za Afrika

Spishi za mabara mengine

Picha

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads